Habari

Waziri Kigwangalla ampa shavu la ubalozi shabiki mtoto maarufu zaidi wa klabu ya Man City, Braydon Bent

Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Hamisi Kigwangalla amempa shavu mtoto maarufu nchini Uingereza, Braydon Bent kwa kumuomba kuwa balozi wa utalii Tanzania.

Image result for kigwangalla
Waziri Kigwangalla

Waziri Kigwangalla ametoa shavu hilo, kupitia ukurasa wake wa Istagram ambapo pia amemkaribisha mtoto huyo kuja kutalii Tanzania kwa gharama ya serikali.

Thank you @braydonbentpage. As a Minister of Tanzanian Natural Resources and Tourism, I would like to welcome you to Tanzania, at our cost, and to appoint you our goodwill ambassador; if you accept the offer, we will appreciate if you would kindly contact me personally on my numbers which @johnjackson_jj shall give you.“ameandika Kigwangalla.

Braydon Bent ni moja ya mashabiki maarufu zaidi wa klabu ya Man City na amekuwa akitumia kiswahili na kuitaja Tanzania katika video zake ambazo zimekuwa zikiwekwa kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Bongo5 imeongea na mtu wa karibu wa familia ya mtoto huyo ambaye pia ni mtangazaji wa Radio Jembe FM, John Jackson amesema kuwa tayari ameshawasilisha maombi hayo ya Waziri Kigwangalla kwa wazazi wa mtoto huyo, na leo watatoa taarifa rasmi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents