Michezo

Waziri Kigwangalla atia neno baada ya Rwanda kuingia makubaliano na PSG ”Tanzania tumefuatwa na vilabu kadhaa”

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla amefunguka baada ya Rwanda kuingia makubaliano na miamba ya soka Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain Football Club kuwa sehemu ya timu ambazo zitakuwa zikisaidia kuutangaza utalii wa nchi hiyo.

Image result for waziri kigwangalla

Kupitia akaunti yake ya kijamii ya Instagram, Dk Kigwangalla ameandika kuwa amepokea malalamiko na ushauri mwingi kufuatia Rwanda kusaini dili na PSG, na kuongeza kuwa Tanzania imefuatwa na klabu kadhaa lakini wanachambua kabla ya Serikali kuamua.

”Nimekuwa nikipokea malalamiko na ushauri mwingi kufuatia ndugu zetu wa Rwanda kusaini dili na @PSG_English. Tunafahamu nguvu na nafasi ya soka ya ulaya kwenye kutangaza brands. Tanzania tumefuatwa na vilabu kadhaa, bado tunachambua kabla Serikali haijaamua kama tuingie ama la. #TanzaniaUnforgettable,” ameandika Waziri Kigwangalla.

Mapema wiki hii Rwanda ilitangaza kuingia makubaliano ya misimu mitatu na klabu kubwa nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG) ambayo itasaidi kuutangazia ulimwengu maliasili, utalii, utamaduni, mazingira na vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika nchi hiyo.

Nchi hiyo inatumaini ushirikiano huo na PSG ambayo inawachezaji wakubwa na maarufu duniani kama Neymar, Mbappe na wengine basi itakuwa chachu ya kufungua milango kwa wafanyabiashara kutoka Ufaransa na kona zote za dunia zitatumia fursa ambazo zinapatikana Rwanda kwaajili ya uwekezaji.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rwanda kuingia makubaliano na klabu za soka katika kuhakikisha inatumia fursa ya ushabiki wa mpira katika kutangaza utalii na vivutio vyake, bali ilishafanya hivyo hata kwa timu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu England na mpaka sasa kwenye jezi ya The Gunneres lipo neno ambalo linasema ‘Visit Rwanda’ na baadhi ya wachezaji wamekuwa wakienda.

https://www.instagram.com/p/B4FkzX8AiF5/

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents