Habari

Waziri Kigwangalla awajia juu watu wa mazingira, Adai wanachelewesha maendeleo kisa mradi wa magari ya umeme (Cable Cars) ya kupanda mlima K/njaro

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla ameshindwa kuvumilia kauli ya Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba akiieleza TANAPA kuwa hawawezi kuanza mradi wa kutumia magari maalumu ya umeme (Cable Cars), kwa ajili ya watalii kupanda katika mlima Kilimanjaro hadi Wizara itakapojiridhisha kwa madhara yatakayotokana na mradi huo.

Akihoji pingamizi hilo kutoka kwa Wizara ya Mazingira, Waziri Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema ni mara ngapi? Watu wa mazingira wanaweka Makongamano lakini bado miti inaendelea kukatwa? Hivyo haoni sababu ya kuhoji mradi mzuri kama wa Cables Car kwani hauharibu mazingira.

Watu wa mazingira wanataka kuingilia kati mradi wa cable cars KILIMANJARO. Lengo letu ni kukuza utalii, kuongeza mapato na kuboresha experience ya watalii wetu nchini. Tusipokuwa wabunifu tunatukanwa kutokutumia vizuri vivutio vyetu, tukiamka wanakuja ‘speed governors’.” Ameandika Kigwangalla na kuhoji.

Mlolongo wa regulative mechanisms zimeua biashara zetu na kukwamisha uwekezaji kwa muda mrefu sana hapa nchini. Hivi sasa tunajaribu kuondoa vikwazo ili kukuza uwekezaji na uchumi wetu. Nchi zinazokua kwa kasi zimeepuka sana njia hizo za kimagharibi. Hivi kuna nchi ngapi zimeweka cable cars kwenye milima yake?Hizi haziharibu mazingira? Cable inapita juu inaharibu mazingira gani? Zaidi ya ekari 350,000/- za misitu zinapotea kila mwaka nchini, ipi ni risk kubwa? ‘Watu wa mazingira’ wamechukua hatua gani zaidi ya makongamano tu?,”ameandika Kigwangalla na kuelezea faida ya kutumia Cable Cars .

Watalii watakaotumia cable cars na wale wa hiking ni tofauti. Hii ni product nyingine, itazalisha ajira nyingine zaidi bila kufuta ajira zilizopo sasa! Wanaopanda kwa cable car kwa uzoefu wetu ni wazee, watoto na familia ambao hawana muda mrefu wa ku-hike.

Kwa upande mwingine, Waziri Kigwangalla amesema endapo kutakuwa na mlolongo mrefu wa kukamilisha mradi huo kutoka kwa watu wa mazingira basi wataachana na mradi huo, Ingawaje ungeingizia taifa watalii milioni 2 kila mwaka baada ya kukamilika.

Vikao vinachelewesha maendeleo! Mtu akiweka kikwazo tunaachana na mradi, tunafanya mengine! Kazi zipo nyingi na muda ni mchache. Tunataka kufikia mwakani tufikishe watalii 2,000,000/-. Mradi mmoja ukituchukulia muda hatutoweza.” ameeleza Kigwangalla.

Kwa upande wa Mhe. January Makamba yeye amejibu kuwa alichoongea sio mtazamo wake binafsi bali ni kutokana na sheria zinavyotaka hivyo asingeliweza kujibizana mitandaoni na Waziri mwenzie Dkt. Kigwangalla.

Serikali imekusudia kujenga mradi huo wa Cable Cars kwa lengo la kuongeza watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro kwa mwaka.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents