DStv Inogilee!

Waziri kumkabidhi Nancy nyumba

Nancy Sumari
2006-04-28 08:13:20
By Renatha Msungu

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, atamkabidhi nyumba mrembo wa Tanzania na Miss World Africa 2005, Nancy Sumari, katika sherehe itakayofanyika Mei 3, kwenye nyumba hiyo iliyoko Tabata, Dar es Salaam.

Nancy alitwaa taji hilo mwaka jana katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania kabla ya kushiriki mashindano ya dunia na kutwaa taji la Miss World Africa.

Mkurugenzi wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, alisema sherehe hizo pia zitahudhuriwa na warembo mbali mbali ambao walishiriki katika kinyang’anyiro hicho.

‘Sasa hivi tuko katika maandalizi ya mwisho ya sherehe ya kumkabidhi nyumba yake…hii itatoa changamoto kwa warembo wengine kujitahidi katika mashindano yajayo,’ alisema Lundenga.

Wakati huo huo, Lundenga alisema Nancy anatarajia kuondoka leo kuelekea Nairobi, Kenya, kwa ajili ya kufanya maandalizi ya safari yake ya kwenda bara la Asia.

SOURCE: Nipashe

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW