Habari

Waziri Lugola kuyafungia Makanisa na Misikiti yenye migogoro

Waziri Lugola kuyafungia Makanisa na Misikiti yenye migogoro

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa atayafungia Makanisa na Misikiti yote ambayo itakuwa na migogoro ya kugombea uongozi na sadaka katika nyumba hizo za ibada ambazo zipo maalum kwaajili ya kuubiri amani na utulivu.

”Na ninataka niwaambie, moja wapo ya ugomvi inayoibuka Misikitini na Makanisani ukiulzia ati wanagombe sadaka, zaka, wanagombea uongozi na nitumie fursa hii kwasababu umezuka mtindo mizozo Makanisani uchonganishi ni kemee jambo hili na jambo hili linamkera Mkuu wa Nchi Rais Dkt  John Pombe Magufuli,” amesema waziri Lugola.

Waziri Lugola ameongeza kuwa ”Anataka kuwe na amani aliyoahidi kuilinda anaposikia migogoro Makanisani, Misikitini afurahi tendo hili na kwakuwa mimi ameniteu kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ninayesajili Makanisa na Misikiti kuanzia sasa Makanisani au Misikitini yatakayo kumbwa na migogoro na migogoro ambayo wameshindwa kuitatua wao wenyenye Misikiti hiyo, Makanisa hayo nitakwenda  kuyafuta mara moja.”

Lugola ameyasema hayo wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Free Pentekoste Jerusalem City lililopo Wilayani Arumeru, mara baada ya kuzindua Tamasha la kuombea amani nchini ambalo limefunguliwa rasmi katika Kanisa hilo, Mkoani Arusha.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents