Habari

Waziri Lugola sakata la Mo: Mtu anaweza tekwa kisa siasa, uchumi, mapenzi na njaa (Video)

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mfanyabiashara Mohamed Dewji na hadi sasa watu 20 wanashikiliwa kusaidia upelelezi.

Waziri Lugola akizungumza na wanahabari amelitaka jeshi la polisi kufanya haraka katika upelelezi wake na kutomshikilia mtu kwa zaidi ya 24.

Amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.

“Sababu za matukio ya kutekwa yanayotokea ni pamoja na kisiasa, kiuchumi, kimapenzi na njaa ili mtu apate fedha na sababu za kutekwa kwa Mohamed Dewji zitajulika hapo wahalifu watakapojulikana” Amesema Lugola.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents