Habari

Waziri Lukuvi kumchukulia hatua aliyempa Makonda shamba

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara aliyemkabidhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda eneo kwa ajili ya viwanda kwa sababu eneo hilo si lake ni mali ya Serikali.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo Jumatatu hii katika mkutano wake na wanahabari. “Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu,” amesema Lukuvi

Aidha Lukuvi amesema anataka watu wote wanaomiliki maeneo mijini kujisalimisha kwa maofisa ardhi wa wilaya wa ajili ya uhakiki.

By: Emmy Mwaipopo

Chanzo: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents