DStv Inogilee!

Waziri Majaliwa amtumbua afisa forodha kwa tuhuma za biashara ya magendo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amuagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kagera, Adam Ntogha kumsimamisha kazi Afisa wa Forodha katika mpaka wa Mulongo Peter Mtei kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za magendo.

Kwa mujibu wa Azam tv, Majaliwa amesema kuwa biashara za magendo zimekuwa zikifanyika bila kuchukua hatua jambo ambalo linatia haibu.

“Biashara za magendo zinafanyika bila ya wao kuchukua hatua, mnatia aibu yaani hakuna kazi inayofanyika,”

”Viongozi wa wilaya ya Kyerwa mjipime wenyewe, mialo mingi katika wilaya yenu inatumika kwa biashara ya magendo na butura.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa katika mwalo wa Mulongo ulipo kwenye eneo ambalo Tanzania inapakana na nchi za Uganda na Rwanda, biashara za magendo na butura zinafanyika na hakuna kiongozi wanaochukua hatua.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW