HabariUncategorized

Waziri Makamba afafanua alichohojiwa na polisi kuhusu kutekwa kwa Mo Dewji

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amefunguka kwa kusema kwamba ni kweli alihojiwa na jeshi la polisi kama anachochote anakijua kuhusu kutekwa kwa bilionea Mo Dewji ambaye aliachiwa Jumamosi hii na watekaji.

Mapema leo taarifa zilianza kusambaa mitandaoni kwamba waziri huyo kijana amekamatwa na baadaye kuthibitishwa na Kamanda wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa.

Makanda apema leo baada ya taarifa hizo kuzagaa alitweet “Sijakamatwa na polisi. Niko salama,”

Baada ya tweet hiyo, alitoa ufafanuzi zaidi kwa kuandika “Polisi walinipigia simu kuniomba, kama rafiki wa Mo Dewji, niwasaidie kama kuna chochote cha ziada ambacho Mo aliniambia kinachoweza kusaidia uchunguzi. Niliwaeleza. Wakasema kinafanana na alichowaeleza. Wakanishukuru. Wamefanya hivi pia kwa wanafamilia. Sikukamatwa.,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents