Habari

Waziri Mkuchika awapa kibano waajiri serikalini

Serikali kupitia Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imewaagiza waajiri wote wa serikali kuhakikisha wanatoa vielelezo vinavyotakiwa vya watumishi wao ndani ya siku 14 pale wanapoagizwa kufanya hivyo na Tume ya Utumishi wa Umma, kinyume cha hapo watawajibishwa.

Waziri George Mkuchika alitoa alipotembelea Tume hiyo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa huku akiwata waajiri hao kuzingatia sheria.

“Waajiri zingatieni sheria, pale tume inapotaka kupata vielelezo inataka ijiridhishe. Kesi zinachukua muda mrefu kama hakuna vielelezo lazima zichelewe,” alisema Mkuchika.

Hata hivyo Mkuchika kwa upande mwingine, aliwataka wafanyakazi wa tume hiyo kutekeleza majukumu yao ya kazi, huku wakijiepusha na rushwa kwasababu eneo wanalofanyia kazi lina ushawishi mkubwa.

Oktoba 7 mwaka huu Rais Magufuli alifanya mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri, Mh. Mkuchika amechukua nafasi ya Waziri Angellah Kairuki ambaye kwasasa ni Waziri wa Madini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents