Habari

Waziri Mkuu aibua mazito ushirika wa Mbinga

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amebaini madudu kwenye vyama vikuu vya Ushirika vya Mbinga (MBICU na MBIFACU) na kuagiza uchunguzi ufanyike kuanzia leo.

Ametoa agizo hilo jana jioni Ijumaa, wakati akiwa anahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbinga, kwenye viwanja vya CCM, mjini Mbinga.

“Nikiondoka hapa jukwaani, Viongozi wote wa zamani na wa sasa waripoti kwa Mkuu wa Wilaya, na OCD hakikisha ofisi za chama hazifunguliwi hadi kesho asubui (leo)’ kazi itakapoanza, ili wasije kubadilisha nyaraka kwenye ofisi yao. Timu yangu ya uchunguzi ikohapa Mbinga, kesho waende wote kwenye ofisi hizoo,”alisema huku akishangiliwa na wananchi.

Alisema timu timu hiyo ya uchunguzi itakiangalia chama hicho na kukifumua chote, na wote wakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kinidhamu. Tunataka MBICU na madeni yenu yaliyoko kwa Msajili wa Hazina yajulikane, tunataka turudishe hoteli yetu, mashamba yetu na majengo yetu, alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma kwa kutembelea wilaya ya Nyasa ambako atazungumza na watumisHIi na madiwani, ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents