Habari

Waziri Mkuu aipongeza Jumuiya ya Kikristo kwa kupanga kujenga makao makuu Dom

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amesema amefurahishwa na uamuzi wa Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wa kutafuta viwanja Dodoma, ili wajenge ofisi za makao yao makuu pamoja na makazi ya viongozi wao wakuu.

whatsapp-image-2016-10-27-at-15-19-37

Ametoa kauli hiyo Alhamisi hii, wakati akizungumza na Askofu mkuu Beatus Kinyaiya, wa Jimbo Katoliki la Dodoma pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kikristo ya huduma za kijamii (CSSC), Peter Maduki, ofisini kwake mjini Dodoma.

whatsapp-image-2016-10-27-at-15-19-34

“Sina shaka juu ya maombi yenu ya kupatiwa viwanja kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu pamoja na makazi ya viongozi wakuu. Sasa hivi Master Plan ya Dodoma kama makao makuu ya nchi inapitiwa upya ili izingatie mahitaji ya msingi sababu zamani ilikuwa haijapangwa kwa mazingira ya sasa ya ujio wa Serikali,” alisema Majaliwa.

Amesema wiki tatu zilizopita alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ili atafute makampuni yenye uwezo wa kupima viwanja kwa haraka. “Hii itatusaidia kutambua tuna eneo kiasi gani na mahitaji halisi ni yapi na nani akija apewe eneo lipi kulingana na mahitaji yake,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Waziri mkuu ameyashukuru makanisa kwa huduma za kijamii zitolewazo katika sekta za elimu, afya na kilimo kama ambavyo ameshuhudia katika baadhi ya maeneo alikopita hapa nchini.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents