Habari

Waziri Mkuu atembelea mradi wa kusafirisha umeme

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa kusafirisha umeme mkoa wa Lindi amesema changamoto ya kukatika umeme katika mkoa wa Lindi kuwa historia baada ya kukamilika kwa mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 Mtwara -Lindi.

Waziri Majaliwa amesema hayo Alhamisi hii, alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi.

“Mikoa wa Lindi ulikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme, kukamilika kwa mradi huu ni mkombozi kwetu, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa tunanishati ya uhakika,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema kuimarika kwa upatikanaji wa umeme kutawezesha safari ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents