Habari

Waziri Mkuu atoa agizo kwa Dkt. Tizeba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemtaka Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba kukutana na wadau wa kilimo ili kufanya mapitio ya gharama za usafirishaji wa mbolea.


Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa katikati akikagua shughuli ya usafirishaji wa mbolea kwenda mikoani kutoka katika ghala la Mohamed Interprises lililopo Mbagala. kushoto kwa Waziri Mkuu ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mohamed Interprises (Mohamed Dewji).

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati akikagua usafirishaji wa mbolea kwenye maghala makubwa matatu jijini Dar es Salaam.

Aidha amesema Serikali inahitaji kuona wakulima wote nchini wanapata pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea kwa wakati ili kilimo kiweze kuwaletea tija.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na usafirishaji wa mbolea kutoka wa wasambazaji wa pembejeo nchini kwenda kwa wakulima.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Kilimo awasiliane na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbawala ili malori yanayobeba mbolea yakifika kwenye vituo vya mizani yapewe kipaumbele.

“Si kwamba yaongeze uzito hapana, bali yapewe kipaumbele cha kupima haraka ili yaweze kuwahisha mbolea kwa wakulima kwani tayari msimu umeshaanza,” alisema Waziri Mkuu.

Maghala aliyoyakagua Waziri Mkuu ni ghala la Mohammed Enterprises lililoko Mbagala, ghala la Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) lililoko Kurasini na ghala la Premium lililoko Vingunguti ambako kote amekuta malori yakipakia mbolea kwa ajili ya uisafirisha katika mikoa mbalimbali nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents