Habari

Waziri Mkuu atoa somo kwa wanafunzi wa kike

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule mbalimbali nchini kusoma kwa bidii na wasikubali kushawishika.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana na WAMA Sharaf,shule ambayo ipo wilayani Lindi inamilikiwa na Taasisi ya WAMA ambapo inasomesha watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira magumu.

“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikubali kushawishika na kukatisha masomo yenu,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wa kike kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa bidii na hatimaye watimize malengo yao.

Waziri Mkuu hata hivyo alikumbusha kuwa Serikali imeweka sheria kali kwa wote watakaobainika kukatisha masomo ya watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito au kuwaozesha.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete alisema shule hiyo inasomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka mikoa yote nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents