Habari

Waziri Mkuu atoa usahihi wa taarifa baada ya kuvunjwa Mamlaka ya CDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa kama kuna mtu alilipa fedha za kiwanja katika Mamlaka ya Ustawi wa Makao makuu Dodoma(CDA) iwe nusu au anataka kumalizia ataendelea kukamilisha malipo yake na kama kuna mtu alishakamilisha hakukabidhiwa kiwanja atakabidhiwa kiwanja chake.

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi baada ya mbunge wa Singida Martha Mrata kuhoji;

Kwa kuwa tarehe 15 mwezi wa 5 mwaka huu serikali ilitangaza rasmi kuivunja Mamlaka ya Ustawi wa Makao makuu Dodoma na majukumu yake kuhamishiwa manispaa ya Dodoma kwahilo naipongeza serikali, lakini kwa kuwa baadhi ya wananchi hata wabunge walikuwa tayari wameshalipia viwanja na walikuwa hawaja kabidhiwa, Je, serikali inatoa tamkoa gani kuhusu jambo hili.

“Ni kweli Mheshimiwa Rais alitoa agizo la kuvunjwa Mamlaka ya CDA na mamlaka hizo na majukumu yake kuzihamishia ofisi ya Tamisemi kupitia manisapaa ya Dodoma kazi hiyo imeshafanywa zoezi linaloendelea sasa kwanza wale watumishi wote wa CDA watahamishiwa manispaa ya Dodoma lakini tutafanya mchujo kidogo wale ambao walikuwa na malalamiko wanalalamikiwa na wananchi wale watu tutawaweka pembeni kwasababu tunataka tupate timu mpya ambao inafanya kazi vizuri,” alisema Majaliwa.

“Lakini mbili tunaendelea na uhakiki na ukaguzi wa kina wa masuala ya fedha na utumishi wenyewe ili tuweze kuanza vizuri tujue CDA ilipoacha iliacha na fedha kiasi gani na shughuli zake ziliishia hatua gani alafu pia kuweza kuendelea lakini majukumu yote yanabaki kama yalivyokuwa CDA yaliendelea kufanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kinachobadilika pale ni maandishi kwenye risiti zilikuwa zinasomeka CDA sasa zitasomea Manispaa baada ya kukamilisha utaratibu huu mpango kazi utaendelea kama ulivyokuwa kama kuna mtu alilipa nusu anataka kumalizia wataendelea kukamilisha malipo yao kama kuna mtu alishakamilisha hakukabidhiwwa kiwanja atakabidhiwa kiwanja chake.”

“Namna yoyote ya utendaji wa kawaida utaendelea sasa hivi akaunti zote zimefungwa kwahiyo huwezi kulipa mpaka hapo tutakapo fungua malipo na tutamuagiza Mkurugenzi wa Manispaa atoe maelezo sahihi kwa wana Dodoma na kwa wananchi na waheshimiwa Wabunge mkiwemo ili kila mmoja weze kujua lakini kwa kauli hii ndo usahihi wa taarifa ya CDA kwa namna ambavyo tumeivunja na tunaamishia Mamlaka pale Manispaa ya Dodoma na watumishi wote sasa watawajibika kwa mkurugenzi wa Manispaa na hakutakuwa na chombo kingine chochote pale.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents