Habari

Waziri Mkuu awataka wanafunzi kuheshimu sheria za vyuoni

Mkutano wa tatu, kikao cha 13 umeendelea leo asubuhi bungeni kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kujibu maswali ya wabunge ya papo kwa papo.

33C8AD8A00000578-3570857-image-a-77_1462273649809

Waziri Mkuu amesema kuwa kila mtu ana haki na uhuru wa kujiunga na chama cha siasa anachokitaka lakini asivunje sheria za sehemu husika.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tarime Mjini kupitia CHADEMA, Esther Matiko aliyeuliza swali kwanini wanafunzi wa vyuo wanaopinga chama cha mapinduzi wanakuwa wananyanyaswa vyuoni hasa chuo kikuu cha Dodoma.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu, Majaliwa amesema sio kweli kama kuna maelekezo yoyote yaliyotolewa na serikali kuwanyanyasa wanafunzi ambao hawaiungi mkono CCM na kwamba kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote ilimradi afuate sheria za mahali husika.

“Mtumishi yeyote au mwanafunzi ana haki ya kujiunga na chama chochote lakini lazima afuate sheria. Tanzania hii ni yetu sote na kila mmoja ana uhuru wa kujiunga na chama chochote anachotaka na serikali itaendelea kuwahudumia wananchi wote bila kujali vyama vyao,” aliongezea.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wanafunzi na watumishi wa umma kuheshimu sheria za sehemu husika hasa kutojihusisha na siasa wakati wa masomo na makazini ili kujiepusha na migongano isiyokuwa ya lazima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents