Habari

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awaonya wakulima

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewaonya wakulima wa ufuta wasikimbilie kuuza zao hilo kwa wanunuzi wasio rasmi maarufu kwa jina la chomachoma bali wasubiri minada itangazwe mwezi ujao.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua uwanja mpya wa michezo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

“Ninawasihi msikubali kuuza kwa akina chomachoma bali tumieni Mfumo wa Stakabadhi za Mazao Ghalani, tumeona mfumo huu ulivyosaidia kwenye korosho,” amesema Waziri Mkuu.

“Kuna wawakilishi wa Kampuni ya Hyseas International Investment (T) Limited ya kutoka China ambao wamekuja hapa kuonana na uongozi wa Halmashauri. Wamesema watanunua ufuta wote uliolimwa Ruangwa na Nachingwea, ndiyo maana ninawasihi msubiri, msikimbiile kuuza ufuta kwa sasa,” alisisitiza.

Alisema kampuni hiyo imeahidi kuweka vituo vya ununuzi kwenye kata za Mandawa, Nanjaru, Nangurugai, Machang’anja hadi Mbangala ili wakulima wasihangaike kusafirisha ufuta wao. “Tunataka mwaka huu, wakulima wa ufuta nao wapate hela nzuri,” alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu alikabidhi mikopo kwa wajasiriamali 42 wanaofanya kazi zao wilayani Ruangwa ambapo kati yao wakina mama lishe ni 39 na wakina baba lishe ni watatu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents