Habari

Waziri Mkuu kuongoza maadhimisho ya walemavu wa ngozi (Albino) Kitaifa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza Maadhimisho ya Kitaifa ya uelewa juu ya ulemavu wa ngozi, albino, ambayo yatafanyika katika viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma ambayo yataanza tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu.


Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Nemes Temba (katikati), kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam Bw.Gabriel Aluga na kushoto ni Afisa Mawasiliano na Habari wa chama hicho Bw. Josephat Torner.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi,albino, Tanzania, Nemes Temba alisema bila utaratibu mzuri wa upatikanaji Takwimu hawataweza kupata takwimu sahihi.

Temba alisema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuibua mijadala na kutafakari juu ya ukusanyaji endelevu wa takwimu,uchambuzi na upatikanaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi kwa wakati ili Serikali iweze kuwasajili.

“Bila ya utaratibu mzuri wa upatikanaji wa Takwimu, Serikali haitaweza kupanga vyema juu ya ustawi wa watu wenye ualbino, hivyo maadhimisho ya mwaka huu yataibua mjadala wa umuhimu wa upatikanaji wa takwimu sahihi kutoka ofisi ya Taifa ya takwimu, kwaajili ya kusaidia katika mipango ya maendeleo ya watu wenye ualbino,”alisema Temba.

Aidha alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 iliyojumuisha takwimu za watu wenye ulemavu wa ngozi, ilisaidia kubaini idadi ya watu hao ambapo walikuwa 16,376 wakiwemo Wanaume 8,763 na Wanawake 10,070.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ‘Takwimu na Tafiti kwa Ustawi wa Watu Wenye Ualbino’, yatahudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wadau toka Sweden, Uholanzi, Marekani, Canada, Uingereza, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Mataifa mengine.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents