Habari

Waziri mkuu Majaliwa amekiri kupokea malalamiko juu ya utendaji usioridhisha wa TRA

Waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa amekiri kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara juu ya utendaji usioridhisha wa mamlaka ya mapato na kuongeza kuwa tatizo lililopo ni TRA kutokufuata kanuni na taratibu za ukusanyaji kodi.
waziri-mkuu-kassim-majaliwa

Mh Majaliwa ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo hapo ambapo amewataka wafanyabiashara au wawekezaji wenye malalamiko juu ya baadhi ya watumishi wa TRA waende kwenye chombo chochote cha usalama ili serikali itafute dawa sahihi ya dawa ya watumishi wa TRA ambao hawafanyikazi zao vizuri.

Waziri mkuu amelazimika kueleza hayo baada ya wabunge kudai kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi ya wafanyabiashara juu ya utaratibu unaotumiwa na TRA kutoza kodi ikiwemo kuwalimbikizia madeni.

Wakichangia mapendekezo ya pango wa maendeleo wa taifa mwaka 2017/18 baadhi ya wabunge mbali na kupendekeza maeneo yanayotakiwa kufanyiwa maboresho ikiwemo kuboresha sekta ya kilimo wamtaka waziri wa fedha kutoa maelezo juu ya madai ya uchumi kukua ili hali wananchi hali ni mbaya.

Awali kipindi cha maswali kwa waziri mkuu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe amewatuhumu wabunge wa CCM kupewa rushwa ya sh milionio 10 ili wapitishe mswada wa huduma za habari hoja iliyokataliwa na naibu spika ambaye alimtaka waziri mkuu asijibu swali hilo kwa madai siyo la kisera.

Source: ITV

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents