Habari

Waziri Mkuu Majaliwa awataka MaRC kufuata sheria katika kutekeleza majukumu yao

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema viongozi hao wa mikoa watazingatia kikamilifu mipaka ya madaraka yao na kwamba hatua watakazozichukua katika uongozi na utendaji wao zitazingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo nchini.

“Mkadumishe uhusiano mwema baina yenu na watumishi walio chini yenu, kwa kuzingatia kuwa kila mtumishi anao mchango katika kuboresha utendaji kwenye kituo chake cha kazi. Nina matarajio makubwa kuwa mtadumisha uhusiano mzuri kikazi na viongozi wa juu na pia uhusiano wa diplomasia ya heshima na viongozi wengine ndani ya mihimili yetu mitatu.”

Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wahakikishe kila mmoja wao anaandaa mpango kazi unaoainisha shughuli zake za kila siku. “Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Wakuu wa Idara wote na Watumishi wote wawe na mpango kazi wa utekelezaji wa majukumu yao.”

Amesema viongozi hao wanatakiwa wasimamie nidhamu kazini na uwajibikaji wa watumishi kwa wananchi, ambapo pia amewasihi watende haki kwa wananchi na watumishi walio chini yao. Pia lazima watumishi wa Serikali wawapokee na kuwahudumia wananchi kwa staha, wawasikilize kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

“Tunakumbushwa sisi viongozi tuhakikishe tunaziendeleza rasilimali za nchi hii kwa faida ya Watanzania wote bila kubagua jinsia, kabila, dini, rangi ya ngozi, mtu atokako ndani ya nchi ilimradi hajavunja sheria, wala ubaguzi mwingine wa aina yoyote. Tunaaswa tuwahudumie Watanzania wote kwa usawa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents