Burudani ya Michezo Live

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda atamani Rais Magufuli kuongezewa muda wa Uongozi (+Video)

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Mizengo Pinda ameeleza matamanio yake kuona Rais John Magufuli anaongezewa miaka mingine mitano baada ya kumaliza muda wake wa uongozi wa miaka 10.

 

Pinda aliyekuwa waziri mkuu mwaka 2008 hadi 2015 ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 12, 2019 katika ufunguzi wa semina ya wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Mwanza.
“Mimi napata matumaini makubwa sana kwamba miaka hii kumi uliyopewa itatupeleka pazuri sana, ni kwa kuwa tu katiba zenyewe kidogo ziko tight lakini kama si kwa sababu hiyo wallah ningesema mzee piga mingine tena ongeza kama mitano tu.”
“Sasa najua hata mkijaribu kumlazimisha atawakatalia tu, lakini nataka niseme kwa namna ninavyoguswa na kazi kubwa unayoifanya,” amesema Pinda.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW