Habari

Waziri Mkuu wa Australia asema mabaki ya ndege ya Malaysia yameonekana kusini mwa bahari ya Hindi

Australia imesema vitu viwili vinavyohusiana na na ndege ya Malaysia Airlines, MH370 iliyopotea, vimeonekana baharini.

dn-abbott-wide-20140320142647355176-620x349

Hatua hiyo ni baada ya msako wa karibu wiki mbili wa ndege hiyo iliyokuwa na 239 pamoja na wafanyakazi wake. Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbott ameliambia bunge la nchi yake kuwa ‘habari mpya na za uhakika’ za satellite zimepatikana ambapo ndege zilikuwa zimeelekezwa kuitafuta katika bahari ya Hindi.

Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilipotea March 8 na ilikuwa ikielekea Beijing.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents