Burudani ya Michezo Live

Waziri Mkuu wa Ethiopia ashinda tuzo ya amani ya Nobel

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mjini Oslo akitoa wito wa kuwepo umoja huku machafuko ya kikabila yakiitikisa nchi yake na juhudi za suluhu pamoja na Eritrea zikionyesha kukwama.

Norwegen l Verleihung des Friedensnobelpreis an Abiy Ahmed in Oslo (picture alliance/AP Photo/NTB scanpix/H. M. Larsen)

Abiy Ahmed mwenye umri wa miaka 43 ameshinda tuzo ya amani ya Nobel kwaajili ya juhudi zake za kuupatia ufumbuzi mzozo wa muda mrefu kati ya Ethiopia na Eritrea.Tuzo hiyo ni jaza pia kwa juhudi zake za upatanishi katika Afrika mashariki na mageuzi ya kidemokrasi aliyoyaanzisha nchini mwake, nchi iliyokuwa ikitawaliwa na waimla kwa muda mrefu.

Akikabidhiwa tuzo hiyo Abiy amesifu mchango wa kiongozi wa Eritrea aliyemtaja kuwa “mshirika na ndugu katika juhudi za amani.”.Tunatambua nchi zetu si maadui. Badala yake ni wahanga wa adui wa pamoja anaeitwa umaskini. Amesema waziri mkuu wa Ethiopia.

“Amani inahitaji imani kuweza kuleta neema, usalama na fursa njema, sawa na jinsi miti inavyomeza gesi ya carboni na kuyapatia maisha yetu hewa safi. Amani ina uwezo wa kumeza dhana zote mbaya zinazoweza kuchafua uhusiano wetu.”Amesema waziri mkuu wa Ethiopia.

Medaali ya dhahabu ya Nobel

Kamati ya Nobel inazungumzia umuhimu wakuendelezwa juhudi za amani

Akimkabidhi tuzo hiyo mwenyekiti wa kamati ya amani ya Nobel Berit Reiss-Andersson amekumbusha shauku iliyokuwa awali imeanza kutoweka na waziri mshindi huyo wa tuzo ya amani anakabiliwa na changamoto kubwa. Mpaka kati ya nchi hizo mbili umefungwa na suala la mpaka bado mpaka sasa halijapatiwa jibu.”Ni matumaini ya kamati ya Nobel ya Norway kwamba yaliyofikiwa awali yakishadidiwa na tuzo ya amani ya Nobel yanachangia kutekeleza makubaliano ya amani-ameongeza kusema bibi Berit Reiss-Andersson.

Sherehe za kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel zimeingia dowa kwa kukataa waziri mkuu Abiy Ahmed kujibu masuala ya vyombo vya habari.

Tuzo  ya amani ya Nobel ni mchanganyiko wa medali ya dhahabu na kitita cha Kron milioni tisa za Sweeden ambazo ni sawa na Euro 850.000.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW