Habari

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi afariki dunia


Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amefariki duniani akiwa na umri wa miaka 57. Kituo cha televisheni cha serikali kimetoa taarifa hiyo baada ya kuwepo wiki kadhaa za wasiwasi kuhusiana na afya yake.

Zenawi alilazwa hospitali mwezi uliopita ambapo ugonjwa uliokuwa unamsumbua haujawekwa wazi. Wasiwasi kuhusiana na afya yake ulianza baada ya kushindwa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa mapema mwezi uliopita.

Waziri huyo mkuu alichukua madaraka kama kiongozi wa waasi kutoka kwa kiongozi wa kikomunisti aliyeondolewa madarakani Mengistu Haile Mariam mwaka 1991.

Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn, ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje atashikilia uongozi wa nchi hiyo kwa muda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents