Habari

Waziri Mkuu wa Israel awekwa kitimoto na Polisi

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu huenda akashtakiwa na Polisi nchini humo kwa mashtaka ya rushwa. Polisi wamesema kuwa wana ushahidi wa kutosha kumtia hatiani kiongozi  huyo kwa rushwa, ufisadi na kuvunjwa uaminifu.


Netanyahu anatuhumiwa kutaka gazeti la Yediot Aharonot kuchapisha taarifa yake yenye upendeleo ili kuliwezesha gazeti hilo kuweza kushindana na magazeti mengine kibiashara. Madai mengine ni kwamba kiongozi huyo alipokea zawadi ya dola 283,000 kutoka kwa msanii wa Hollwood Mogul Arnon Milchan ili kuweza kumsaidia kupata Visa ya Marekani.

Polisi wanasema mhariri wa gazeti la Yediot Aharonot, Arnon Mozes na Milchan ambaye ni mtayarishaji wa filamu nao pia watashtakiwa kwa tuhuma za rushwa.

Hata hivyo Benjamin Netanyahu amekanusha tuhuma hizo na kusema madai hayo hayana msingi wowote na ataendelea kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo, wakati huo huo vyombo vya habari nchini humo vikieleza kuwa tayari Netanyahu amehojiwa mara zisizopungua saba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents