Tupo Nawe

Waziri Mkuu wa Mali ajiuzulu pamoja na baraza zima la mawaziri

Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali amekubali ombi la kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Soumeylou Boubeye Maiga na Baraza lake zima la mawaziri.

Waziri Mkuu Soumeylou Boubeye Maiga

Soumeylou Boubeye Maiga alichukuwa hatua hiyo hapo jana, kufuatia wiki mbili za maandamano ya umma dhidi ya mauaji ya kiholela katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

“Rais ameridhia maombi ya kujiuzuru kwa Waziri Mkuu huyo na wajumbe wengine wa Serikali. Mbadala wa Maiga atatangazwa muda wowote kuanzia sasa.” Ofisi ya Rais ilitoa kauli hiyo hapo jana siku ya Alhamisi.

Maandamano hayo yalichochewa na mauaji ya wachungaji 160 wa jamii ya Fulani, ambayo yanashukiwa kufanywa na watu wa jamii ya Dogon, wanaoishi kwa kilimo na uwindaji.

Prime MInister Soumeylou Boubeye Maiga in New York (Reuters/E. Munoz)

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ujerumani, Deutsche Welle, Mauaji hayo yaliitikisa Mali, ambayo katika miezi ya karibuni imeshuhudia mauaji mengine kadhaa, yakiwemo yale ya wanajeshi 23 walioshambuliwa kwenye kituo chao.

Juzi Jumatano, bunge lilijadili uwezakano wa kura ya kutokuwa na imani na Serikali kutokana na mauaji hayo na pia kushindwa kuwanyang’anya silaha na kuwazuwia wanamgambo wa itikadi kali.

Umoja wa Mataifa una zaidi ya wanajeshi 16,000 nchini Mali, vikiwemo vikosi kutoka Ufaransa na Ujerumani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW