Burudani

Waziri Mwakyembe aagiza Nandy akamatwe, Adai Diamond bado anahojiwa na polisi kwa kusambaza video chafu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema  kuwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz jana Aprili 16, 2018 alikamatwa na polisi na kuhojiwa kuhusu video zake chafu alizosambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Tokeo la picha la mwakyembe bungeni
Waziri Mwakyembe

Waziri Mwakyembe amesema hayo leo Aprili 17, 2018 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlingwa aliyehoji jinsi gani serikali imejipanga kupambana na wasanii wa muziki pamoja na vikundi vya watu wanaosambaza lugha za matusi.

Waziri Mwakyembe amesema “Tulitunga sheria mwaka 2010 lakini tulikosa kanuni za kuweza kubana hasa maudhui upande wa mitandao, tumeshatunga hizo kanuni na sasa hivi hizo kanuni zimeanza kufanya kazi. Kuna baadhi ya wasanii wetu ambao walianza kufanya uhuni uhuni ndani ya mitandao ya kijamii jana tumeweza kumkamata msanii nyota Tanzania Diamond na tumemfikisha polisi na anahojiwa kutokana na picha chafu alizozirusha vile vile inabidi hata binti Nandy naye akamatwe ahojiwe,“amesema Waziri Mwakyembe.

Kwa upande mwingine Waziri Mwakyembe amewaonya vijana kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii ambapo amesema kuwa mitandao hiyo ni vyema ikatumika vizuri kwa masuala ya maendeleo na sio kuharibu utamaduni wetu.

Jana kwenye mitandao ya kijamii kulisambaa video ya msanii Diamond Platnumz akiwa faragha na wanawake wawili tofauti tofauti akiwemo mzazi mwenzake Hamissa Mobetto kitu ambacho kiliibua mijadala kibao wengi wakidai kuwa amewadhalilisha wanawake.

Soma zaidi – Mashabiki wamshambulia Diamond, Wadai amefanya udhalilishaji kwa wanawake

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents