Tupo Nawe

Waziri Mwakyembe ageuka Mbogo sakata la TFF kumtimua kocha Amunike ‘Viongozi wa Shirikisho na nyie mjiuzulu’

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewaomba viongozi wa TFF waeleze sababu za kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike.

Waziri Mwakyembe kulia kwenye picha.

Waziri Mwakyembe ameeleza hayo jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, Na kuhoji kuwa kama wameiga kutoka kwa Misri basi na wao wajiuzulu.

Sijui msingi wa kumuondoa Amunike ni upi, si kwamba mimi nilikuwa namtaka wala simhitaji, lakini nataka kila kitu kiende kwa utaratibu na ndiyo maana nataka kuwahoji msingi wa kumuondoa Amunike ni upi?. Kama tunaiga walichofanya Misri basi tuige sawasawa kwamba baada ya kumwambia kocha aondoke inabidi na wewe kiongozi wa shirikisho na wenzako muondoke.“ameeleza Mwakyembe na kudai kuwa hapingani na Shirikisho kumfukuza Amunike ila anataka sababu za kumfukuza.

Hatupingi kilichotokea ila mpango wa TFF ni upi kutupeleka hatua nyingine, au tunaiga kilichotokea Misri, kama tunaiga basi tuige sawa kwamba baada ya kumwambia kocha aondoke inabidi na wewe kiongozi wa shirikisho na wenzako muondoke,” amesema Mwakyembe.

Kwenye mkutano huo viongozi wa TFF hawakuhudhuria licha ya kualikwa na Waziri huyo mwenye dhamana na michezo nchini.

Mapema wiki hii, Shirikisho la soka nchini (TFF) lilitangaza kumfuta kazi kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike bila kutoa sababu za msingi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW