Tupo Nawe

Waziri Mwakyembe asema ni marufuku uwanja wa taifa kuita kwa mchina ‘Hatukupewa zawadi na mchina, nikisikia nataka kutapika’

Wakati akizindua nembo itakayotumika kwenye michuano ya Afcon kwa vijana waliyo na umri chini ya miaka 17, itakayo fanyika hapa nchini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka waandishi wa habari pamoja na Watanzania kutouita uwanja wa taifa kwa Mchina.

”Mimi niwaombe wanahabari wa magazeti, radio na luninga tuwe waangalifu katika kuanzisha misemo na vibwagizo kwenye michezo ambayo inaweza kupotosha na kuto isaidia kulijenga Taifa,” amesema Waziri Mwakyembe.

Hata hivyo, Dkt. Mwakyembe ameongeza ”Imejitokeza mtindo wa kuita uwanja wa Taifa kwa mchina, mimi naomba ni seme tu moja kwa moja huu ni upuuzi uliyopitiliza, nawaomba msiuwite uwanja huu kwa mchina.”

”Uwanja huu hatukupewa zawadi na mchina, usijenge mtazamo kwa watoto kwamba tulipewa zawadi na mchina, unatukana kodi ya Mtanzania.”

”Tafadha, nikisikia nataka kutapika, basi tuseme tukutane kwa Mkapa ndiyo mzee wetu aliyejenga inawasumbua nini mpaka mkamtaja mchina ?.”

”Ndiye mzee wetu aliyeanzisha huu uwanja, sawa ni kibwagizo kizuri lakini linatudhalilisha kama Watanzania, nimeskia zaidi ya mara nne, mara tano kwa mchina kwa mchina, kwa mchina wapi ?.”

Dkt. Harrison Mwakyembe amewashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW