Michezo

Waziri Mwakyembe atembelea nyumbani kwa mchezaji wa Serengeti Boys(Video+Picha)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb), hapo jana amepata fursa ya kumtembelea na kumjulia hali aliyekuwa nahodha wa timu ya Serengeti Boys Issa Abdi Makamba nyumbani kwao katika kitongoji cha Mlezi, Dodoma.    Issa ambaye aliumia mguu wa kulia wakati akiwa katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya AFCON nchini Gabon.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison  Mwakyembe (kushoto) akiwa na mchezaji wa timu ya Serengeti Boys Issa Abdi Makamba nyumbani kwao katika kitongoji cha Mlezi, Dodoma.

 

Mhe. Mwakyembe alitumia fursa hiyo kumpa pole na huku akimhakikishia mchezaji huyo huduma muhimu hadi afya yake itakapotengemaa.

Aidha, Mhe. Mwakyembe alimwambia Serikali bado haijawatupa mkono waliokuwa wachezaji wa Serengeti Boys na sasa wanaandaliwa utaratibu ili wawekwe kambini na kuandaliwa hatua nyingine .

 

Kwa upande wake Issa alimshukuru Mhe. Mwakyembe kwa uamuzi wake wa kwenda kumtembelea nyumbani licha ya kuwa na majukumu mengi.

“Nakushukuru Mhe. Waziri kwa kuonyesha utu na kuja kunitembelea na kujionea hali yangu, kwani tangu nimerudi nyumbani sijawahi kuwaona viongozi wa mchezo wa mpira wa miguu nchini” alisisitiza Issa.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents