Habari

Waziri Mwakyembe atoa neno kwa Watanzania

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amewashukuru Watanzania wote waliomfariji katika msiba wa mke wake mpendwa Linah Mwakyembe.

Aliyazungumza hayo katika misa ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwake Kyela mkoani Mbeya, Dkt Mwakyembe amesema kuwa amefarijika sana kwa upendo ulioonyeshwa na kila mtu kwa nafasi yake.

“Mimi na wanangu tumefarijika sana kwa kuona jinsi ambavyo watanzania na wana Kyela mlivvyokuwa na upendo kwetu mmetupa faraja na mmetutia nguvu na mmetuonyesha ushirikiano mkubwa katika jambo hili tunaomba mwenyezi Mungu awabariki sana na asanteni sana”Amesema Waziri Mwakyembe.

Julai 15, Mke wa Mwakyembe alifariki dunia na amezikwa jana Kyela Mbeya.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents