Michezo

Waziri Mwakyembe atoa neno zito saa chache kabla ya uchaguzi TFF

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewataka wajumbe wa mkutamno mkuu wa TFF kuwa makini katika kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wa Shirikisho hilo kwakuwa wao ndiyo tumaini la watanzania.

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dk. Harrison Mwakyembe

Mwakyembe ameyasema hayo mkoani Dodoma ambapo uchaguzi wa viongozi mbali mbali wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania unaendelea.

Katika uchaguzi huo wapo pia wageni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA na lile la Afrika Caf wakiwa wanafuatilia kwa makini namna mchakato wa kupata viongozi wapya wa TFF unavyoendeshwa.

Baadhi ya wajumbe kutoka FIFA

Dkt Mwakyembe amesema kuwa TFF inahitaji viongozi watakao walea watoto wenye vipaji vya soka walioibuliwa katika mashindano ya hivi karibuni na watakao weza kusimamia mfumo wa leseni za klabu.

Wagombea wa nafasi ya Rais wa TFF

“Ndugu wajumbe viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usioteteleka kwa vishawishi vya mpito, serikali inaamini tuna wajumbe makini huku ndani wasioyumbishwa na vishawishi vya muda na vishawishi vya mpito, tunataka viongozi wanaongozwa na uzalendo wa hali ya juu, hivyo tunataka viongozi bora wa TFF wenye hali, moyo, uelewa, weledi na uadilifu unaotakiwa kupeleka soka letu mbele” alisema Mwakyembe

Lakini pia amewaomba wajumbe kuchagua uongozi utakaoshirikiana na serikali kufanya maandalizi ya mashindano ya vijana  wenye umri usiozidi miaka 17 ambayo yatafanyika hapa nchini 2019 #UchaguziTFF.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents