Michezo

Waziri Mwakyembe aushukuru uongozi wa SportPesa baada ya kutembelea uwanja wa Taifa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa eneo la kuchezea mpira (picth) la Uwanja wa Taifa wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas (mwenye shati jeupe wapili kutoka kwa Waziri)

 

Akizungumza katika ziara hiyo ya kukagua hatua iliyofikiwa katika matengenezo ya uwanja huo.

Waziri Mhe.Dkt. Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya awali ya ukarabati na anatarajia mabadiliko makubwa zaidi baada ya hatua zinazofuata kukamilika .

“Nimefurahishwa na mabadiliko niliyoyaona katika hatua hii ya awali naamini ukarabati utakapokamilika milango itakuwa wazi kwa mechi za kimataifa ikiwemo mashindano ya AFCON yanayoratajiwa kufanyika nchini kwetu mwaka 2019” alisema Dkt.Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha viwanja vingine vikiwemo vya mikoani vinafanyiwa ukarabati ili kuboresha sekta ya michezo nchini.

Waziri Dkt. Mwakyembe ameushukuru uongozi wa SPORTPESA kwa kuonyesha ushirikiano wa karibu na Serikali katika kuhakikisha inaweka mchango wake katika michezo kwa kukarabati sehemu ya kuchezea mpira (picth) ya Uwanja wa Taifa pamoja na vifaa mbalimbali vilivyotolewa katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas ameeleza kuwa kampuni yao imefanya hivyo ikiwa ni njia ya kuonyesha uzalendo wa kupenda na kuthamini vya nyumbani.

“Hatua hii ni ya awali baada ya mechi ya Everton na Gorimahiya mnamo Julai 13 mwaka huu hatua itakayofuata ni ya kuondoa nyasi zote na kuotesha mpya ambazo zitachukuwa miezi mitatu kuwa sawa” alisema Bw.Tarimba.

Uwanja wa Taifa ulianza matengenezo ya eneo la kucheze (pitch) rasmi katikati ya mwezi wa sita lengo ni kuhakikisha nyasi zilizochakaa zinaondolewa na kuwekwa nyasi mpya zitazodumu zaidi ya miaka 10.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents