Michezo

Waziri Mwakyembe awatia nguvu Serengeti Boys

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Dr. Harrison Mwakyembe, Leo Jumamosi Januari 20, 2018 ameitembelea timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 16 Serengeti Boys iliyopo kambini kwenye hostel za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF na kuwaachia ujumbe wa Serikali.

Dr. Mwakyembe akitoa salamu za Serikali amewaambia Vijana wanaounda timu hiyo kuwa serikali inawaamini na wanalo jukumu la kuiperusha vyema bendera ya Tanzania.

Amewataka kupambana kwaajili ya Tanzania na kuhakikisha wanafanya vyema kwenye kila mashindano huku akiwataka makocha wa kikosi hicho kuwapa mafunzo mazuri kwa ustawi wa Vijana hao.

Aidha Dr. Mwakyembe amesema anaamini Vijana hao watakuwa bora chini ya TFF iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Ndugu Wallace Karia.

“Naamini mtaimarika na kuwa bora maana hata TFF hii sasa ina ari na morali kubwa”.Alisema Dr. Mwakyembe.

Katika ziara yake hiyo Dr. Mwakyembe alipata nafasi ya kutazama mchezo wa kirafiki kati ya Serengeti Boys na Makongo Sekondari iliyomalizika kwa Serengeti Boys kupata ushindi wa mabao 4-1.

Kabla ya mchezo huo Serengeti Boys walicheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Kituo cha Bombom iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents