BurudaniUncategorized

Waziri Mwakyembe azindua Bodi ya BASATA na ishu ya maadili kwa wasanii, FA na Single waanza kazi (Video)

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) Jumatano hii amezindua rasmi Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) chombo chenye jukumu la kusimamia utendaji wa tasisi hiyo ambayo inajukumu kubwa la kusimamia sanaa nchini Tanzania.

Mhe. Rais John Pombe Magufuli alimteua Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhe Habi Gunze naye Waziri Mwakyembe kuwateua wajumbe wa bodi hiyo akiwemo rapa Mwana FA pamoja na muigizaji, Single Mtambalike maarufu kwa jina la Richie.

Waziri Mwakyembe na bodi ya BASATA

Akizungumza katika uzinduzi huyo, Dkt. Mwakyembe wameitaka bodi hiyo kwenda kuisimamia Basata kutenda kazi zake kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa pamoja na kuanza kukufua vyanzo vipya vya mapato kwa baraza hilo ili kukuza sanaa pamoja na uchumi wa nchi.

Waziri alizindua Bodi hiyo kwa kuchoza kwenye ubao picha za hao model waliovalia magazeti.

“Sekta ya sanaa inachangamoto nyingi ikiwemo suala la mmomonyoko wa maadili katika kuendesha shughuli za sanaa kwa baadhi ya wasanii na wadau wa sanaa. Suala hili limekuwa likijitokeza mara kwa mara ambapo baadhi ya wasanii wamekuwa wakiandaa na kufanya kazi za sanaa zisizo na staha na maadili,” alisema Waziri Mwakyembe.

Aliongeza, “Hatuna budi kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa kwa kuweka miongozo thabiti ya kusimamia suala la maadili. Ninaelewa changamoto hii huchangiwa sana na kupitwa na wakati kwa sheria ya BASATA Na. 23 ya 1984 ambayo huelezea BASATA kama mlezi na sio mdhibiti na mwendelezaji. Suala hili wizara yangu italifanyia kazi kwani hatuwezi kuendelea kuona wasanii wetu wamekuwa ni sehemu ya kujunja maadili yetu tena kwa makusudi,”

Kwa upande wa Mwenyekiti wa bodi hiyo alisema wao wamezipokea changamoto hizo na wanakwenda kuzifanyia kazi mara moja ili kuleta sura mpya kwa baraza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents