Michezo

Waziri Mwakyembe azitaka kampuni za kubashiri kusaidia sekta ya michezo na kuipongeza SportPesa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka wamiliki wa Kampuni za Michezo ya Kubahatisha kujitokeza kwa wingi na kusaidia ukuaji wa sekta ya Michezo.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokutana na viongozi wa makapuni mbalimbali ya mchezo wa kubahatisha nchini  kwa lengo la kuzungumza nao kuhusu kuchangia sekta ya michezo kwa maendeleo ya taifa kama inavyofanyika katika mataifa mengine.

”Ningependa msaidie kukuza sekta ya michezo nchini na Imani kwa kufanya hivyo michezo itakuwa kwa kasi kubwa,” amesema Dkt. Mwakyembe

Waziri Mwakyembe ameongeza “Najua nyinyi ni wadau wakubwa wa michezo japo mchezo huu wa kubahatisha ni mgeni katika taifa letu ila ni mchezo unaokuwa kwa kasi hivyo ningependa kuona mnatoa ushirikiano katika kukuza sekta ya michezo kwa taifa kwani sekta ya hii imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa fedha na miundombinu.”

Pamoja na hayo Waziri huyo aliendelea kutoa shukrani kwa mchango uliyotolewa na moja ya Kampuni ya Mchezo wa kubahatisha ya Sportpesa kwa kutoa ufadhili wa kufanya matengenezo ya nyasi za uwanja wa Taifa zilizokuwa zimechakaa kufuatia maandalizi ya mashindano ya AFCON Under 17 ya 2019 yatakayofanyika nchini.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Waendesha Michezo ya Kubahatisha (TSBA) Bw.Dhiresh Kaba aliahidi serikali kuwa shirikisho liko tayari kutoa  ushirikiano katika kuisaidia sekta ya michezo na sababu wanatambua umuhimu wa michezo kwa taifa.

“Naishukuru Serikali kwa kutupa nafasi ya kuweza kuchangia katika ya maendeleo ya michezo nchini sababu mchezo wetu unategema sana michezo na michezo ya nchini itakapopata mafanikio  itatusaidia na sisi kuongeza wigo wa mchezo huu wa kubahatisha.”amesema Bw.Kaba.

Hata hivyo michezo ya kubahatisha ni mmoja ya sekta inayokuwa kwa kasi nchini hivyo kupitia mchango wao wanaweza kusaidia kuboresha miundombinu ya michezo ambayo imekuwa na changamoto nyingi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents