Michezo

Waziri Mwakyembe: Vijana wangu naomba mzingatie vitu vitatu

Hafla ya uzinduzi wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake imezinduliwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kwenye Uwanja wa General Tyre jijini Arusha.

 

Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Twiga Stars, Edna Lema akiteta na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Uwanja wa General Tyre, katika mchezo wa ufunguzi Alliance Queens wameshinda 2-1 dhidi ya Panama FC.

Katika uzinduzi huo Waziri Dk. Mwakyembe aliwataka wachezaji wa timu zote kujituma kwa juhudi zaidi kwa kuwa mpira wa miguu kwa sasa ni ajira kubwa sana kwa vijana.

“Vijana wangu natambua mnapenda mpira wa miguu, naomba mzingatie vitu vitatu muhimu – nidhamu, juhudi na kujitunza,” amesema Waziri Dk. Mwakyembe akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred na viongozi wa FA Mkoa wa Arusha

Mara baada ya kufanya uzinduzi huo, Waziri akiwa na viongozi hao leo ametembelea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutazama maendeleo ya marekebisho yanayofanyika kwenye Uwanja huo.

 

Mbali na uwanja  huo pia waziri alifanya ziara fupi kwenye viwanja wmbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanja cha FFU kwa Morombo, Arusha  ambapo aliwapongeza kwa ukarabati mzuri wa nyasi za kuchezea.

Katika ziara nyingine Waziri pamoja na Viongozi wa TFF walitembelea shule ya Trust St. Patric Sports Academy ambacho ni kutuo cha kukuza michezo na timu zinazoshiriki ligi hiyo, zimeweka kambi.

Timu zilizokata utepe zilikuwa ni Alliance Queens ya Mwanza iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Panama FC ya Iringa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents