Habari

Waziri Nchemba aagizwa kusitisha kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kusimamisha kutowapa uraia wakimbizi wa Burundi.

Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo, wakati wa ziara yake mkoani Kagera, akiwa na mgeni wake Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ambapo amewaomba wakimbizi kurudi nchini kwao kwa hiari.

“Kwa hiyo na mimi nawaomba wakimbizi kwa hiari yao warudi Burundi mimi siwafukuzi ila kwa hiari yao warudi nyumbani. Nimesikia wakimbizi wengine wameahidiwa kupewa elfu kumi kumi wabaki sasa nasema wakawapeni hizo hela mkiwa Burundi,” amesema Rais Magufuli.

“Rais amezungumza hapa kwa upole, Rais mwenyewe ana hofu ya Mungu, wazazi wake waliuawa, lakini anataka kushirikiana na Warundi wote kwa nini mnataka kuondoka kwenu.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents