Habari

Waziri Nchemba apokea tani 230 za Cement ujenzi wa nyumba za polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba amepokea tani 230 za cement kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari polisi na tani 130 kwa ajili ya ujenzi wa hospital na mabweni ya wanafunzi katika jimbo la iramba kutoka kiwanda cha simba cement cha jijini Tanga.

Waziri Nchemba amewashukuru kiwanda cha simba kwa kuchangia shughuli za maendeleo ya jamii hasa kusaidia serikali katika ujenzi wa nyumba bora za askari polisi na ujenzi wa hospital na mabweni na kusema kuwa ni mfano wa kuigwa nchini

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo jijini Tanga katika kiwanda cha simba cement na kuwataka watanzania na wafanyabiashara wenye uwezo kuchangia shughuli za maendeleo nchini kama kujenga vituo vya polisi, nyumba za askari polisi,magereza na zimamoto ili kuwapa morali ya kazi zaidi vijana wanaofanyakazi masaa 24 kulinda raia na mali zao.

“Mimi kama waziri nawashukuru sana simba cement kwa kuisaidia wizara yetu zaidi ya mifuko 5500 kwa ajili ya kusaidia polisi pemba ujenzi wa nyumba za askari ambao wanaishi katika mazingira magumu sana rai yangu kwa watu wenye uwezo tunawakaribisha,” alisema Dkt. Mwigulu

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha Simba cement, Mhandisi Reinhardt Swart amesema wao kama kampuni huwa wanasaidia sana shule zikizo katika mkoa wa Tanga lakini sasa wameamaua kusaidia Taasisi zingine za serikali amabazo zinauHitaji wa kuboresha miundombinu kama wanavyofanya kwa polisi pemba na shule na hospital za Iramba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents