Habari

Waziri Nchemba atoa onyo kwa mwananchi atakayekosa kitambulisho cha Taifa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa Tanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari ni lazima kwa mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambuliwa.

Amesema hayo akizindua zoezi la kujiandikisha kuoata kitambulisho cha Taifa na kugawa vitambulisho katika mkoa wa Ruvuma na kukagua zoezi hilo linaendaje kwa mikoa ya nyanda za kusini hasa iliyoko mipakani mwa nchi.

Waziri mwigulu amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania.

Waziri Nchemba amewagiza viongozi wa wilaya na vijiji kutokuunganisha zoezi la kuandikisha wananchi kupata vitambulisho vya uraia na zoezi lingine lolote akitolea mfano baadhi ya viongozi kuchangisha fedha za kijiji kwa kuwaambia kuwa hutopata kitambulisho mpaka utakapo lipa fedha unazo daiwa na kijiji.

Naye Kaimu Mkurugenzi mkuu wa vitambulisho vya Taifa Andrew masawe amesema zoezi la kuandikisha wananchi linatakiwa kuisha ifikapo mwezi December 2018 huku akitaja changamoto wanazokutana nazo kuwa ni la viambatanisho vile vinavyoonyesha umli wa mtu na makazi kwani wananchi huwa hawaendi navyo wakat wa kujiandikisha.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema wao kama mkoa wamejipanga kila wilaya wataendesha zoezi hilo kwa kushirikiana na taasisi zingine kama uhamiaji kuwatambua raia halali wa Tanzanaia.​

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents