Habari

Waziri Nchemba atoa siku 7 kwa Warundi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 7 kwa shirika la wakimbizi nchini Tanzania kukamilisha taratibu za wakuwarudisha Warundi walioomba kwa ridhaa yao kurudi kwa nchini Burundi.

Waziri Nchemba amechukua hatua hiyo baada ya kupata taarifa kuna watu 8743 ambao wamesajiliwa kwa hiari yao kurudi Burundi waliopo katika kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma lakini hawakuhamishwa na shirika la UNHCR ambapo wanasema wanataka kukaa kikao ili waweze kuwarudisha.

“Natoa siku 7 kuanzia leo muwe mmeshakamilisha utaratibu nan mniambie hilo kundi la kwanza linaanza kuondoka lini na yanandoka mfululizo mpaka lini au yanaondoka lini au waliojiandikisha wawe wameondoka kama zitapita siku 7 hamjafanya hivyo nitaongea na pacha wangu Waziri wa Ulinzi amuombe Amiri Jeshi Mkuu ili tupate magari ya Jeshi ndo yapeleke hao watu kwao,” alisema Mwigulu.

“Hatuwezi tukapambana na watu wanaotaka kwenda kwao na tukitumia magari ya jeshi kuwapeleka nyinyi sijui mtatafuta ofisi sijui mtatafuta ofisi sijui mtaziweka wapi tukitafuta watu wa kufanya kazi hiyo sijui nyinyi mtakuwa mnafanya nini hizi excuse za kusema kuna consult Rais wao siamesema hapo na wao wameitikia.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents