Habari

Waziri Nchemba atoa taarifa ya mwaka 2017 (+Video)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dkt.Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa Tanzania kuwa mbele ya matukio kabla hayajatokea ili yaweze kudhibitiwa.

Dkt Nchemba ameyasema hayo leo akiongea na waandishi mkoa wa Dodoma akitoa muelekeo wa wizara yake kwa mwaka mpya wa 2018 nini kama wizara wamejipanga kufanya.

Waziri Nchemba amesema matukio ya mauaji yaliyotokea mwaka uliopita mengi yamelipotiwa polisi baada ya matukio kutokea lakini huko nyuma watu walikuwa wanajua kuhusu kutishiana kwa kutoa kauli ambayo mbaya bila kutoa taarifa polisi.

Kuhusu kuotwa kwa miili mingi maeneo ya baharini na baadhi ya maeneo nchini, Waziri huyo amesema miili hiyo ilikua ya wahamiaji haramu amabao walikuwa wanasafirishwa nje ya nchi na wahamiaji hao walikuwa wanasirishwa katika magari hayana hewa wanabebwa kama mahindi wakifa kwa kukosa hewa na hakula wanatupwa sehemu mbalimbali ili wanaowasafirsha wasikamatwe na sehemu nyingine polisi wanawakamata wahamiaji wakiwa hoi sana.

Waziri Mwigulu amesema kwa mwaka huu wamejipanga kwa kuweka hatua kali akitokea mtu kawabeba hao watu atachukuliwa hatua kali na chombo kilichobeba hao watu kitataifishwa.

Waziri Nchemba amewataka wananchi kuto kuchukilia kawaida taarifa za kupotea kwa watu zaidi ya wiki bila kutoa taarifa kwa kudhani kuwa atakua mahali fulani kwa kudhani kuwa hakuna ubaya unaweza kutokea hata wahusika wanaotishwa wasichukulie kirahisi tu watoe taarifa polisi.

“kwa mwaka 2017 matukio yaliyoniudhi zaidi ni tukio la kushambuliwa kwa askari polisi na wananchi maeneo kibiti na kushambuliwa kwa kiongozi mda wa mchana tena katikati ya mji wa serikali na watu kupotea sehemu kusiko julikana hivyo nawataka wananchi kuwa mbele ya matukio kwa kutoa taarifa na kama wizara sisi tupo vitani mda wote kuwasaka waharifu na kuzia uharifu kwa mwaka 2018” Waziri Mwigulu

Kuhusu mlindikano wa wafungwa katika magereza nchini amesema kwa sasa wanapanga kukaa na wizara ya TAMISEMI kuona jinsi ya kuweka utaratibu wa adhabu hata ya kufanya kazi kwa wale ambao wanamakosa madogo kama ya kushindwa kulipa fedha baada ya kufanya kosa madogodogo ili kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani na kwakuweka zaidi ya magerezani ni kuwachangana na wafungwa wazoefu na wanaweza kufundishwa kufanya makosazaidi.

Waziri Nchemba amesema kwa mwaka 2018 kauli mbiu ya wizara yake itakua ni kila Mtanzania kushirikiana kuwa mbele ya matukio kwa kutoa taarifa ili kudhibiti uharifu kabla ujatokea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents