Habari

Waziri Nchemba awaomba viongozi wa dini kupiga vita dawa za kulevya

Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba,amewaomba viongozi wa dini nchini kupiga vita dhidi ya dawa za kulevya.

nchemba1

Ameyasema hayo mjini Dodoma akifungua mkutano wa kanisa la kiinjiri la kilutheri, KKKT.

“Ninyi mna nafasi kubwa ya kutusaidia dhidi ya kupiga vita madawa ya kulevya, ninyi mpo kila eneo, nyinyi hamuhongeki, nyinyi hamna fitina, kauli yenu ushuhuda wenu na mtawanyiko wenu, mna msaada sana katika kupambana na dhidi ya madawa ya kulevya,” alisema Nchemba.

“Kwa kufichua wanaofanya hivyo, wapo miongoni mwa wananchi huko tunakoishi,” aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents