Waziri Ngeleja ndani ya Clouds FM

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (pichani kulia) leo asubuhi alialikwa katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na redio ya Clouds FM, kwa lengo la kufafanua mengi kuhusiana na Wizara yake ikiwemo operesheni maalum ya kukusanya madeni ya TANESCO nchi nzima iliyoanza hivi karibuni (kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho Gerald Hando).

Operesheni hiyo ya nchi nzima ina lengo la kukusanya madeni zaidi ya shilingi bilioni 300 kutoka kwa wateja mbalimbali, zikiwemo taasisi za umma na binafsi.

Waziri Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga mara baada ya kumaliza mahojiano ya kipindi cha Power Breakfast.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents