Habari

Waziri Ulega awapa jukumu hili maafisa wa forodha

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka maofisa wa forodha wa Sirari wilayani Tarime kuongeza juhudi katika kulinda rasirimali ili kuunga mkono kasi ya Rais Dk John Mafuguli ya kulinda rasirimali hizo.

Naibu Waziri wa Mifugo, Abdallah Ulega akizungumza na maafisa hao

Ulega alieleza hayo wakati akizungumza na wafanyanyakazi wa forodha hiyo katika kikao kati yake na watendaji baada ya kufanya ziara katika eneo hilo.

Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo, baada ya kuelezwa kwamba wilaya hiyo haina tatizo la mifugo kutoka nje ya nchi na kuingia nchini lakini kumekuwa na tabia kwa baadhi ya madalali kutorosha mifugo na kuuza nchi jirani ya Kenya.

“Hili halikubaliki kabisa kwa sababu kama Serikali tunakosa mapato yanayotoka na mifugo hii endapo ingekuwa inafuata utaratibu wa kupita katika forodha ya hii lakini miekuwa kinyume badala yake inapitishwa kwa njia za panya hadi Kenya,”

Aliwaataka watendaji hao kutobabaika bdala yake wasimamie sheria na kufanya kazi kwa uadilifu ikiwamo kushirikiana ili kudhibiti hali hiyo inarudisha nyuma jitihada za Serikali za kuleta maendeleo.

Pia Ulega alitumia nafasi kuwaeleza watumishi hao kwamba wizara itahakikisha kituo cha ukaguzi wa mifugo cha Kirumi wilayani Butiama kinafanya kazi kwa ufanisi kuwa kuweka miundombinu ya maji na umeme ili mnada uliopo uanze kufanya kazi.

Kabla ya kwenda katika forodha hiyo, Ulega alipat fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na walipeana mikakati mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha sekta ya mifugo na uvuvi inasonga mbele.

Katika mazungumzo yao viongozi hao walikubaliana suala la kudhibiti uvuvi haramu hasa unaofanyika katika ziwa Victoria ambapo Malima alimwahidi Ulega kwamba atahakikisha anatumia vyombo vya dola ili kukabiliana na hali.
Wakati Malima akieleza hayo, Ulega naye alimwakikishia kwamba wizara hiyo itakuswa bega kwa bega kushirikiana na mkoa huo katika kuhakikisha sekta hizo zinapiga hatua na kusonga mbele.

Mbali na hilo, viongozi hao walikubaliana kuanza kwa mchakato wa kufufua viwanda vya kusindika samaki na nyama vilivyopo ili kuunga mkono jitihada za Dk Magufuli za Tanzania ya viwanda ili kuwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents