Habari

Waziri Ummy amshukuru Rais Magufuli

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemshukuru Rais Magufuli kwa kuongeza chachu katika mapambano dhidi ya Malaria kwa kununua lita laki moja na kusambazwa kote nchini.

Shukrani hizo zimetolewa na Waziri Ummy wakati wa ugawaji wa Viuadudu vya kutokomeza Mbu wa Malaria kwa halmashauri kumi na moja zilizofika katika kiwanda cha kuzalisha Viuadudu hivyo kilichopo Mjini Kibaha.

Waziri Ummy alisema anamshukuru Mhe. Rais kwa kumruhusu kuanza zoezi hilo kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza Viuadudu hivyo vitagawiwa kwa Halmashuri 14 nchini ambazo zina viwango vikubwa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria,hii ametupa nguvu na sisi tuliopo kwenye dhamana ya kusimamia sekta ya afya katika kupambana na Malaria.

“Maelekezo yangu hasa kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha dawa hii mnapulizia kuzingatia miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya, muangalie ukubwa wa eneo la mazalia ya mbu,na kiasi kinachotakiwa kupulizia,” alisema Ummy.

Aidha Waziri Ummy amewataka wahakikishe wanapulizia Viuadudu hivyo angalau mara nne kwa mwezi kwa maana kila baada ya siku saba,hivyo ni lazima wanunue vifaa vya kupulizia dawa hii pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi watakaenda kufanya zoezi hilo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents