Habari

Waziri wa Elimu ana madaraka makubwa mno -Haki Elimu

Taasisi ya Elimu isiyo ya kiserikali ya Haki Elimu imepongeza seriakali kwa juhudi ya mabadiliko ya kuondoa mamlaka ya usimamizi wa elimu ya cheti na stashahada kutoka baraza la elimu na ufundi(NACTE) na mamlaka hayo kuwa chini ya wizara na baraza la mitihani la Taifa NECTA huku Mkurugenzi wa taasisi hiyo akisema kuwa waziri wa elimu ana madaraka makubwa.

pichakielimu

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu,John Kalage amesema pamoja na kupongeza jitihada hizo za serikali inapaswa kutambua mabadiliko ya mara kwa mara kuachilia kutokuwepo kwa mipango endelevu ya elimu ambapo taifa litapaswa kuwa na dira pamoja na chombo chenye mamlaka ya kusimamia kanuni,sheria na sera kwa lengo la kuboresha mifumo ya elimu hapa nchini.

“Lakini sasa pamoja na hayo kuna mambo ambayo tunafikiri tunatakiwa kuishauri serikali unapoona mabadiliko ya mara kwa mara kwenye mfumo wa utoaji wa elimu. Hatuna dira nzuri inayoongoza mfumo wa elimu,lakini pia inaathiri uendelevu wa programu zinazoanzishwa inaonyesha kwamba waziri wa elimu anakuwa na madaraka makubwa sana katika kusimamia mfumo wa elimu kwa maana nyingine ni kwamba anapotaka mabadiliko yawe yanakuwepo,”alisema Kalage.

“Leo tunapongeza haya kwasababu ni mazuri lakini kwa mamlaka aliyokuwa nayo ina maana kwa wakati mwingine akiwa na maono mazuri mnaweza mkashangaa yakaja mabadiliko ambayo sisi wengi tutayapigia kelele kwamba haya mabadiliko ya mara kwa mara yanaathiri wa elimu Tanzania,”ameongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents