Habari

Waziri wa Fedha aeleza hali ya ukuaji wa uchumi

Serikali kupitia Wizara wa Fedha na Mipango, imesema katika nusu ya kwanza ya mwaka huu pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana(2016).

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akizungumza kuhusu hali ya uchumi wa Taifa, utekelezaji wa bajeti mwaka 2017/2018.

“Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu pato la taifa limekuwa kwa asilimia 6.8 ukilinganisha na asilimia 7.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2016, sasa hapa nataka nifafanue kidogo kwa wale ambao sio wataalamu ukuaji wa uchumi hauendi wima au kama mstari ulionyooka hata kidogo,” alisema Dk. Mpango.

“Mara nyingi wachumi wanapochora ukuaji wa pato la taifa unaenda kama mawimbi hivi tena mawimbi yenye hayalingani na sababu yake ni rahisi kwasababu kwa mfano kilimo kina msimu amabo ndio tunavuna lakini pia nikitoa mfano mwingine kama utalii kuna msimu wa watalii wengi na kuna wakati ni low season . Haiwezekani uchumi ukawa unapanda .”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents