Tupo Nawe

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi aunga mkono kampuni ya Huawei kudai haki mahakamani dhidi ya Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ameunga mkono uamuzi wa kampuni kubwa ya teknolojia, Huawei kudai haki mahakamani dhidi ya serikali ya Marekani iliyopiga marufuku bidhaa zake akieleza kuwa kampuni za China ‘zisikubali kuonewa kama kondoo’.

Wang Yi amesema kesi zinazoanzishwa dhidi ya kampuni za kichina na raia wake ni njama za makusudi za kisiasa kuivuruga China.

Kwa mujibu wa mashirika mbalimbali ya habari likiwemo Global News limeripoti kuwa Mnamo mwezi Desemba, afisa mkuu wa maswala ya fedha wa Huawei, Meng Wanzhou alikamatwa huko nchini Canada kwa ombi la taifa la Marekani.

Waziri, Wang Yi ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari ambao ni wakila mwaka wa bunge na kusisitiza kuwa ni dhahiri hatua za Marekani ni za kisiasa na makusudi kuwashusha baadhi ya watu na makampuni.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW